MAJALIWA: TUTAENDELEA KUSIMAMIA BEI NZURI YA MAZAO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan itaendelea kusimamia bei nzuri ya mazao kwa wakulima nchini. Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 27, 2021) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwate katika kipindi cha Maswali ya Papi kwa Papo kwa Waziri Mkuu